lugha ya KISUKUMA
jina Wasukuma linatokana na neno “sukuma” lenye maana ya “kaskazini” katika lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi. Wanyamwezi waliwaita “Bhasukuma” yaani watu wa kaskazini mwao. Nao Wasukuma waliwaita Wanyamwezi “Bhadakama”.
Maria Nyanjige akinukuliwa, asema anafafanua kuhusu historia ya Wasukuma, “ kihistoria asili ya kabila la wasukuma ni nchini Ethiopia, na akaongeza kuwa kabila la Wasukuma limegawanyika katika sehemu tatu, kwamba kuna wasukuma wa Mwanza, Wasukuma wa Tabora na Wasukuma wa Shinyanga, akaeleza kuwa pamoja na kugawanyika kwa makabila hayo lakini bado yanalafudhi inayotofautiana kwa namna moja ama nyingine” kuna maelezo yahusuyo makumbusho ya Bujora ambapo tamaduni za Wasukuma zimehifadhiwa. Bujora zamani iliitwa Kujorwaningo kutokana na eneo hilo kuwa hatari kutokana na wanyama hatari na watu wanyongao watu wengine, hivyo eneo hilo likabatizwa jina la kujorwaningo yaani kwa kisukuma kunyonga shingo.
inaelezea kuwa Kisukuma ni lugha ya kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasukuma mwaka 2006, idadi ya wasemaji wa Kisukuma imehesabiwa kuwa ni watu milioni 543000. Kufuatana na Uainishaji wa lugha za Kbantu wa Malcom Guthrie, Kisukuma iko katika kundi la F20. inafanana na lugha ya Kinyamwezi.
Jina “Wasukuma” lina maana ya watu wa “kaskazini” lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsili kwa mfano Wasukuma hutumia alama ya utambulisho kwa eneo fulani kwa viashirio vya makabila kwa mfano jina kama hili: Kiiyalina maana ya mashariki ambako ni mawio ya jua. Huu ni utambulisho ambao haukufanikishwa ama kuitwa kwa jina la kabila fulani mfano mwingine ni upande wa “dakama” ambapo yatambulisha kama eneo la Unyamwezi lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa “kusini” zaidi ya hapo neno hili hutumiwa sana na kabila la Wanyamwezi ili kutambulisha eneo la Wasukuma ambapo Wasukuma nao husema “dakama” upande mwingine ambao unapewa alama ya utambulisho wa neno “shashi” maana yake ni upande wa kabila la “Washashi” na neno hili washashi ni mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa Mara.
Japo pia neno hili “shashi” linamaanisha kabila la Wakurya ambao pia mpanuko wake unakomea hapo ambapo zaidi ya eneo zima la upande huu unamaanisha upande wa kaskazini. Upande wa mwisho kutambulishwa ni “Ngw’eli” neno hili halikupewa kabla na badala yake linamaanisha upande mashariki (dira), ambako ni machweo ya jua. “Wasukuma wenyewe hulirejelea jina hili kama “bhasukuma” kwa umoja “nsukuma”
Wasukuma huishi eneo la kaskazini mashariki mwa Tanzania, karibu na mwambao wa kusini mwa ziwa Victoria na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya Nyamagana. Mkoa wa Mwanza, upo pia kusini magharibi mwa mkoa wa Mara, mkoa wa Simiyu na mkoa wa shinyanga
Eneo la kaskazini la makazi yao ni katika Mbuga maarufu Serengeti familia za wasukuma wengi sana wamehamia maeneo ya kusini kuelekea mkoa wa Rukwa ambako baadae umegawanywa na kuzaa mkoa wa katavi, wakipita maeneo ya kabila la wapimbwe na hivyo kufanya mkazi katika eneo la kijiji cha wapimbwe.
Shughuli za kiuchumi
Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo na uvuvi ufugaji na biashara. Pamba ndio zao kuu la biashara kwa Wasukuma ambao pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku mahindi, viazi, dengu na mahinda (kisiwani ukerewe) wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvivu madini kama vile dhahabu almasi ma madini ambayo huchimbwa katika maeneo mbalimbali mkoa wa Mwanza na Shinyanga.
Wasukuma pia wanajihusisha sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina mbalimbali. Maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama mahindi na mpunga idadi ya watu ina ongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezaeka kwa wakulima na mbogamboga.
Shughuli za sherehe
Wasukuma wengi katika karne ya ishirini, walitumia utamaduni wao zaidi katika kusherehekea matukio ya nyakati mbalimbali kwa mfano wakati wa mavuno, unyago ndoa na misiba. watemi ndio walikuwa viongozi wa kabila la wasukuma na watu walikaa katika eneo moja.
Dhana ya Fonimu
Riro, (2012:60) fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho kina uamilifu wa kutofautisha maana kinapochukua nafasi ya kipashio kingine chenye hadhi sawa.
Massamba (2004:12), fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi cha kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake; sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha.
Naye Mgullu (2012:55) anasema ,fonimu ni kipashio kidogo kabisa katika lugha kilicho na uamilifu wa kutofautisha maana katika maneno. Kwa mfano kutoka katika lugha ya kisukuma unaweza kupata fonimu zifuatazo;
JEDWALI LINALOONYESHA FONIMU KATIKA LUGHA YA KISUKUMA. (KINASUKUMA - MWANZA)
Fonimu za Kisukuma
|
Maana ya Kiswahili
|
Lekaga…./ l/
Sekaga …../s/
Zulaga …../l/
Zugaga…/g/
Enjaga…./Ɉ/
Engaga…/g/
Ngubho…/u/
Ngobho…/ɔ/
|
acha
cheka
vua,
pika
chukua,
ondoka au toka
kiboko (mnyama)
mavazi(nguo)
|
Ø Kuwepo kwa fonimu /l/ na /s/ katika maneno Lekaga na Sekaga zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Ø Kuwepo kwa fonimu /l/ na /g/ katika maneno Zulaga na Zugaga zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Ø Kuwepo kwa fonimu /Ɉ/ na /g/ katika maneno Enjaga na Engaga zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Ø Kuwepo kwa fonimu /u/ na /ɔ/ katika maneno Ngubho na Ngobho zimepelekea kuwepo kwa maana tofauti katika maneno hayo.
Dhana ya Konsonanti katika lugha ya Kisukuma.
Massamba na wenzake (2004: 27) Konsonanti ni aina za sauti ambazo hutambulika kama kuzuia mkondo wa hewa utokao mapafuni kupitia chemba cha kinywa na chemba ya pua kuondoa nje uzuiaji wa mkondo huo wa hewa unaweza kubana kabisa au kuachia ghafla kisha kuachia taratibu kama tunatamka neno /p/
Naye Masebo (2012:89) Konsonanti ni sauti zinazotamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu mbalimbali hasa kwa kutumia ulimi kama vile /p/, /b/ /d/
Kutokana na fasili hizo, Konsonanti ni sauti za lugha ambazo sauti hizo hewa haiondoki mdomoni moja kwa moja lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.
Katika lugha ya kisukuma tunapata Konsonanti zifuatazo kama zinavyoonyeshwa kwenye jedwali lifuatalo;-
JEDWALI KUONYESHA KONSONANTI KATIKA LUGHA YA KISUKUMA (KIMUNASUKUMA- Mwanza)
Konsonanti
|
Kifonetiki
|
Neno/ maneno
|
maana
|
bh
|
[β]
|
Bhabha
Bhose,
Bhochaga
Bhana
Bhanhu
|
Baba
Wote
Beba
Watoto
watu
|
c
|
[]
|
Chene
Chagulaga
Chunghu
|
Hivyo
Chagua
Shimo
|
d
|
[d]
|
Demaga
Dongo
Duba
|
Chunga
Chura
Tupa
|
f
|
[f]
|
Fulaga
Fulaga
Fungulo
|
Fua
Puliza
Funguo
|
ɡ
|
(ɡ)
|
Geshaga
Galukaga
Gojaga
|
Salimia
Geuka
Ngoja
|
h
|
[h]
|
Hambhohambho
Hatale
Hene?
Humulaga
|
Afadhali
Pakubwa
Kweli?
nyamaza
|
j
|
[Ɉ]
|
Jaga
jingaga
Jako
Jongaga
|
Nenda
tongoza
Zako
finya
|
k
|
[k]
|
Keshaga
Kinehe
Kwihebha (kwigusha)
|
Kesha
Vipi
kucheza
|
l
|
[l]
|
Lalaga
Lushiko
Lyaga
Lemi
|
Lala
Siku
Kula
Jua
|
m
|
[m]
|
Minze
Mabhele
Maguta
Mbuli
|
Maji
Maziwa
Mafuta
mbuzi
|
n
|
[n]
|
Nene
naleho
Nzoka
nsumba
|
Mimi
Nipo
Nyoka
kijana
|
p
|
[p]
|
Pelaga
Pungujaga
Pujaga
|
Kimbia
Punguza
Koboa
|
s
|
[ s]
|
Sabhuni
Sibhitali
Sebha
|
sabuni
Hospitali
Mungu
|
t
|
[t]
|
Tolaga
Temaga
Tulaga
Tuja
|
Kuoa
Kata
Piga
dharau
|
w
|
[w]
|
Walwa
Walaga
Wilaga
Wane
wise
|
Pombe
Mtoto wa mwisho
Usiku
Wangu
wetu
|
y
|
[j]
|
Yombo
Yene
Yose
Yunga
|
kelele
ile
Yote
Chekesha
|
z
|
[z]
|
Zugaga
Zumaleka
Zuma
|
Pika
Kufariki
Laani
|
ng’
|
[ŋ]
|
Ng’wangaluka
Ng’wanike
Ng’wana
Ng’wadila
|
Za ahsubuhi
Wasichana
Mtoto
Za jioni
|
ny
|
[ɲ]
|
Nyaga
Nyanda
Nyamu
|
Upepo
Kijana
paka
|
sh
|
[ʃ]
|
Shilewa
Shitambo
Shikombe
Shijiko
|
Chakula
Hatua
Kikombe
kijiko
|
Dhana ya Irabu katika lugha ya Kisukuma
/i/ /u/
/I/ /ʊ/
/e/ /o/
/a /
|
/a/ +irabu
+ kati
+chini
-mviringo
mfano: abhana- watoto
Abhizikulu - wajukuu
Aho – pale
/e/ + irabu
+mbele
+nusu chini
–mviringo
mfano Bhebhe – wewe
chene –chini
engaga – toka
/I/ +irabu
+mbele
–mviringo
+nusu juu
Ijagi –jagi
Idatu- tatu
Ine-nne
/i/ + irabu
+mbele
-mviringo
+ juu
mfano : ipela – pera
idoka – duka
idoke-mgomba
/ ʊ/ + irabu
+nyuma
+mviringo
+nusu juu
mfano: idatʊ– tatu
ʊleja - unaenda
ʊlelya – unakula?
/u/ + irabu
+juu
+nyuma
+mwiringo
Mfano; mabhu-majivu
Miundo ya silabi katika lugha ya kisukuma
Riro (2012: 77). silabi ni dhana ya kifonolojia ambayo huwakilisha umbo la matamshi ambapo sauti moja au zaidi hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja la sauti. Ifuatayo ni Miundo ya silabi katika lugha ya kisukuma
i. Muundo wa Irabu peke yake (I)
mfano:
Ipela – pera
Idatu – tatu
Enzoka – nyoka
Aho – pale
ii. Muundo wa Konsonanti + Irabu (KI)
mfano: Sekaga - cheka
Tolaga – oa
Somaga – soma
iii. Muundo wa konsonanti + konsonati +Irabu (KKI)
mfano:
Embiti – fisi
Ngosha- mwanaume
Chagulaga – chagua
Ntale - mkubwa
Ndoke - ndizi
iv. Muundo wa konsonanti+ kiyeyusho+ Irabu (KI1/2 I)
mfano:
Ulelya- kula
Nyanza – ziwa
v. Muundo wa konsonanti peke yake (K)
mfano:
Mva- mbwa
vi. Muundo wa Konsonanti + Konsonanti + kiyegusho + Irabu (KKI1/2 I)
Mfano;
Nsungwi- sungwi
Ngwala – Ngwara au mtama
DHANA YA ALOFONI KATIKA LUGHA YA KISUKUMA (KINASUKUMA – MWANZA)
Mgullu (2012:59) alofoni ni sauti mojawapo miongoni mwa sauti kadhaa zinazoiwakilisha fonimu moja. Alofoni hutokea katika mazingira mahususi.
Naye Riro (2012:73) alofoni ni maumbo mawili au zaidi ambayo huakilisha fonimu moja. Waidha alofoni ni matamshi tofauti ya fonimu moja ambayo hujitokeza kutegemea mazingira ya utokeaji ya sauti hiyo.
JEDWALI LIFUATALO LINAONYESHA ALOFONI KATIKA LUGHA YA KISUKUMA
Kisukuma Mwanza
|
Kinyantuzu Shinyanga
|
Kinakiiya Simiyu
|
Kiswahili
|
Shikombe
Shitabho
Bhushishi
Shikolo
Shilewa
|
Sikombe
Sitabho
Bhusisi
Sikolo
Silewa
|
Jikombe
Jitabho
Bhosisi
Jikolo
Jilewa
|
Kikombe
kitabu
ukwaju
kitu
chakula
|
LAHAJA KATIKA LUGHA YA KISUKUMA.
Kamusi karne ya ishirini na moja (2013) lahaja ni tawi dogo la lugha Fulani linalozungumzia katika eneo Fulani la kijiografia lengo tofauti za kimatamshi kimuundo matumizi ya maneno kwa mfano; lahaja ya Kiswahili inayozungumzwa Mombasa huitwa kimvita.
Naye Masebo (2012:20) lahaja ni tofauti ndogo ndogo zinazojitokeza katika lugha kuu yenye asili moja. Tofauti hizo zipo katika matamshi (lafudhi) maumbo au matumizi ya maneno.
Katika lugha ya kisukuma kuna lahaja kuu tatu na lahaja hizo zimegawanyika kulingana na maeneo ya kijiografia na lahaja hizo ni kinasukuma, kinyantuzu, kinakiiya.
Lahaja ya Kinasukuma ni lahaja ambayo inazungumzwa na watu wa mwanza na wilaya zake, kimunasukuma ni lahaja inayojulikana kama lahaja ya kaskazini ambayo inatumiwa na watu wa mwanza na wilaya zake kama vile nyamagana, misungwi sengerema na ilemela mfano wa maneno yanayopatikana katika lahaja hii ni:-
magulu- miguu
Miso – macho
Nindo – pua
Lahaja ya Kinyantuzu ni lahaja ya kisukuma ambayo inazungumzwa na watu wa shinyanga na baadhi ya maeneo ya Simiyu kama vile bariadi. lahaja hii inajulikana kama lahaja ya kusini mfano wa maneno ya lahaja ya kinantuzu ni :-
guseka cheka
sinonu – vitamu
solo- moja
nzwele – nywele
gusula – kufua
mdege – mahindi
Lahaja ya Kinakiiyani lahaja ambayo inazungumzwa maeneo ya Simiyu, Bariadi na lamadi, lahaja hii inajulikana kama lahaja ya mashariki, jina la lahaja hii kinakiiya limetokana na neno la kisukuma ambalo ni kiiya lenye maana ya mashariki hivyo basi, lahaja hizi tatu zinatofautiana kwa tofauti za kilekiska na kimfumo
Tofauti za kilekiska.
Hii hutokea pale ambapo fonimu iliyochaguliwa katika neno au maneno kuwa tofauti katika lahaja moja ukilinganisha na lahaja nyingine.
Jedwali lifuatalo linaonesha tofauti za kilekiska katika lahaja za kisukuma.
Kinasukuma (Mwanza)
|
Kinyantuzu (Shinyanga)
|
Kinakiiya (Simiyu)
|
Kiswahili
|
Kwigusha
|
Gwihebha
|
Kwisinya
|
Kucheza
|
Mandege
|
Mandege
|
Mdege
|
Mahindi
|
wabheja
|
Obheja
|
Wabezya
|
Ahsante
|
Wawiza
|
Owiza
|
Mwiza
|
Mzuri
|
Shikolo
|
Sikolo
|
Jikolo
|
Kitu
|
Tofauti za kimfumo
Katika lugha ya Kisukuma, kuna baadhi ya lahaja zinakuwa na sauti /h/ na nyingine zinakuwa hazina sauti hiyo katika mazingira sawa kwa mfano Kinakiiya na Kinyantuzu hazina sauti /h/.
Jedwali lifuatalo linaonyesha tofauti za kimfumo.
Kinasukuma(mwanza)
|
Kinyantuzu(shinyanga)
|
Kinakiiya(Simiyu)
|
Kiswahili
|
Bhagosha
Bhing’we
Kubhona
Shinonu
Shilewa
|
Bagosha
Bing’we
Kobona
Sinonu
silewa
|
Bagosha
Bing’we
Kubona
Jinonu
Jilewa
|
Wanaume
Ninyi
Kuona
Vitamu
Chakula
|
Hitimisho, Kutokana na utafiti huu imebainika kabila la Wasukuma lina wazungumzaji wengi sana wa lugha ya kisukuma katika nchi ya Tanzania mathalani katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita na Simiyu wakati huo wengine wametawanyika katika maeneo mengine ya Tanzania kutokana na mtawanyiko huo shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo ufugaji na uvuvi kama vile Kinasukuma kaskazini Mwanza, Kinyantuzu kusini – Shinyanga, Tabora na Kinakiiya Mashariki – Simiyu.
MAREJELEO
Chubwa, P. (1979). Waha Historia na maendeleo. Tabora: TMP book departiment,
Masebo J. A& Nyangwine N.( 2012). Nadharia ya lugha ya Kiswahili 1: kidato cha 5&6. Dar
es Salaam Tanzania: Nyangwine publishers.
Massamba ,D.P.B (2004). Fonolojia ya Kiswahili sanifu(FONIKISA). Dar es salaam: TUKI.
michuzijr.blogspot.com
Mdee na wenzake (2013). kamusi ya karne ya 21. Dar es salaamu Tanzania: Longhorn.
Mgullu, R.S (2011), Mtalaa wa Isimu: Fonetiki , Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi:
Longhorn
Riro, S. M (2012)Dafina ya lugha isimu na nadharia: kwa sekondari, vyuo vya kati na vyuo
vikuu. Mwanza, Tanzania: Serengeti educational publishers (T) LTD.
ruhuwiko.blogspot.com
lugha ya KISUKUMA
Reviewed by Unknown
on
April 03, 2017
Rating:
No comments