TOFAUTI KATI YA LUGHA YA BINADAMU NA MAWASILIANO YA WANYAMA.
Kwa
mujibu wa Masamba na Wenzake Mwaka (1999: 1) “Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa
madhumuni ya mawasiliano kati yao”.
Pia
kwa mujibu wa NKWERA F.M.V (1979) “Lugha
ni utaratibu (mfumo) maalumu wa sauti za nasibu zenye maana ambazo hutumiwa
miongoni mwa binadamu kwa madhumuni ya mawasiliano miongoni mwao sauti hizi
lazima ziwe za kutamkika”.
Hivyo
basi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali walioeleza maana ya dhana ya Lugha. Lugha ni utaratibu maalumu wa sauti
za nasibu ambazo huodhi maana katika jamii fulani sauti hizi hutumiwa na
wanajamii hao kwa kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao.
Binadamu
hutumia lugha kama nyenzo kuu ya mawasiliano tofauti na wanyama wengine. Kwa
mujibu wa kamusi ya karne ya 21 kamusi ya Kiswahili. “Mawasiliano ni upashanaji wa habari kwa kutumia barua, simu au
vyombo vya habari kama vile redio na televisheni’
Mawasiliano ni
kubadilishana ujumbe (habari) baina ya wawasilianaji mfano, mtu na mtu ama mtu
na kikundi. Pia wanyama huwa wanawasiliana na mawasiliano yao yana husisha
ishara na sauti tofauti na binadamu ambaye hutumia lugha. Hivyo kuna tofauti
baina ya Lugha za binadamu na mawasiliano ya wanyama kama ifuatavyo;-
Uwili;
Lugha ya binadamu huwa na uwili yaani inajitokeza katika viwango viwili Sauti
na Maana katika sauti Mofu, Fonimu, na Lekisimu viwango hivi huunganishwa ili
kupata neno lenye maana tofauti, kwa mfano fonimu maneno
sentensi lakini katika mawasiliano ya wanyama hayawezi kuchanganuliwa
kwa kuanzia kipashio kidogo hadi kikubwa
Lugha ina sifa ya ubunifu au uzalishaji;
Binadamu katika kuzungumza anauwezo wa kubuni na kuweza kuunda maneno mapya na
hata kuzungumza maneno mengi katika kuelezea jambo au mada fulani kwa wakati
mmoja kwa mfano, kutokana na neno lima tunaweza kupata maneno kama vile limia,
limiana, limika, limisha. Maneno haya yana maana tofautitofauti na zinaeleweka.
Tofauti na mawasiliano ya wanyama ambapo
wanyama wanaidadi mahususi za ishara na sauti. kwa mfano ng’ombe anapohisi njaa
hawezi kutoa mlio tofauti na ule aliozoea kuwasilisha ujumbe kuwa ananjaa
anahitaji chakula.
Lugha ya binadamu hutumika ghafla
na kuna kubadilishana zamu; lakini katika mawasiliano ya
wanyama hamna kubadilishana zamu binadamu anaweza kuzungumza maswala mbalimbali
kwa wakati mmoja, pia binadamu hawazungumzi kwa pamoja bali huzungumza kwa
zamu, kunakuwapo msemaji na msikilizaji kwa mfano mahojiano kati ya daktari na
mgonjwa mgonjwa anapomuelezea daktari, daktari huwa ni msikilizaji na wakati
daktari anapomshauri mgonjwa, mgonjwa huwa msikilizaji hivyo hali ya
kubadilishana zamu hutokea. Hali hii ni tofauti na mawasiliano ya wanyama. Mfano
nguruwe wanapoitaji chakula hulia wote kwa pamoja
Umakinikaji;
binadamu huweza kuendelea kuzungumza ilihali anaendelea na jambo lingine mfano
anaweza kuwa analima huku anaongea masuala tofauti na kilimo mfano siasa
,michezo na afya lakini wanyama huzama
katika kile wanachokitenda tu , kwa mfano mbwa anapobweka husitisha shughuli
zote na kuzama katika kitendo cha kubweka.
Unasibu; lugha
ya binadamu haina uhusiano halisi wa dhana ya kirejelewa au kitajwa na hutumia sauti, ishara,
alama na maneno. Mfano neno nyumba halina uhusiano wa moja kwa moja na kirejelewa chake ndio maana
hurejelewa kwa majina tofauti mfano house (kiingereza), enju (kihaya ) na ekhaa
(kiganda) lakini mawasiliano ya wanyama yana uhusiano kwani ishara wanazotumia
mfano paka hukunjua makucha yake kuashiria utayari wake kumshambulia adui wake
. Aidha ni maneno macheche tu yenye uhusiano wa moja kwa moja na virejelewa
vyake mfano nyoka (umbo) na pikipiki (sauti).
Viwango vya uundaji;
katika Lugha binadamu huwa na viwango maalumu vya uundaji kwa mfano, sauti/b/
huunda fonimu/ba/ na fonimu huunda mofimu au maneno/baba/ ambayo nayo pia
huunda kirai (kisu kikali) ambacho huunda kishazi kinachounda sentensi ambayo
huunda kifungu cha habari au habari kamili (kisu kikali kimeibiwa) tofauti na
mawasiliano ya wanyama hakuna viwango vya uundaji.
Lugha ya binadamu huwa na sifa ya
utekelezaji wa majukumu mbalimbali; utekelezaji huu unaweza
kuwa kama vile kusali, kuimba, kutoa nasaha, kutoa
hotuba, ahadi kwa mfano,
baba alimwahidi mwanae kumsomesha. Ila kwa upande wa mawasiliano ya wanyama huwa ni
kufikisha ujumbe tu haitekelezi majukumu tu.
Usambavu;
Lugha
ya binadamu huwa na sifa ya usambavu ambayo humsaidia mwanadamu kuelezea juu ya
vitu vilivyombali kijografia na kihistoria, pia matumizi ya maandishi, maneno
na ishara, Binadamu hutumia maandishi, Ishara na maneno kuzungumzia dhana
yeyote kwa upana wowote ule bila upeo au kikomo pamoja na kuelezea yaliyopita,
yaliyopo na yajayo.hii ni tofauti na mawasiliano ya wanyama kwa sabababu hawana
uwezo wa huu wa usambavu kwa mfano panya hawezi kuwahadisia watoto wake
alivyonusulika kuliwa na paka mwezi uliopita
binadamu huweza kurejelea matukio yaliyopita ya sasa na yajayo.
Hufungamana na utamaduni wa jamii
husika; lugha ya
mwanadamu hurithishwa kizazi kimoja kwenda kizazi kingine kupitia utamaduni wa
jamii husika au utamaduni na mazingira
ambayomtu amekulia , mfano motto yeyote ana uwezo wa kuzungumza lugha yeyote
duniani kutegemeana na mazingira auutamaduniambayo amewekewa kukulia, mfano
motto wa kimasai anapozaliwa ,anapolelewa na kukulia katika utamaduni na
mazingira ya kizungu tofauti na wanyama ambao huzaliwa na mlio ambayo wanaitoa
na wala hawawezi kubadilishana utamaduni na mazingira , mfano hata ng’ombe
akiwekwa na mbuzi hawezi kujifunza utamaduni wa mbuzi wala sauti na ishara za
mbuzi japo wako katika mazingira
yapamoja.
Hitimisho;
kwa mtazamo huu lugha ya binadamu hutofautiana na mawasiliano ya wanyama, hivyo
utofauti hizo zinatokana na sifa bia za lugha. Hata hivyo ni vigumu kuelewa vipengele mbalimbali vya
mawasiliano ya wanyama kwa uwazi unaodhihirika tofauti na lugha ya binadamu kwani wanyama hawana lugha halisi iliyodhahiri
bali huwasiliana kwa ishara tu.
MAREJELEO
Matinde
R.S (2012) Dafina ya Lugha Isimu na
Nadharia, Serengeti Editor Publishers (T) Ltd, Mwanza –Tanzania.
J.S.Mdee,K.
Njogu,Shafi,A. (2011) .Kamusi ya kiswahili
ya karne ya 21,Longhorn Publishers (T) Ltd, Dar es salaam –Tanzania.
TOFAUTI KATI YA LUGHA YA BINADAMU NA MAWASILIANO YA WANYAMA.
Reviewed by Unknown
on
May 15, 2017
Rating:
good work done
ReplyDeleteKazi njema
ReplyDeletegood notes....can i get your link please
ReplyDeleteSwadakta
ReplyDeleteKazi nzuri,kabisaa👍👍
ReplyDeleteKai mufti
ReplyDeleteKongole
ReplyDeleteWell done by Jr Paul
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri kabisa.kongole
ReplyDeleteKazi nzuri kabisa
ReplyDeleteAsante Sana kongole
ReplyDelete