aina za fasihi

kama tujuavyo, fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa. darasa lilipita tuliangalia maana ya fasihi kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali.

leo darasa letu litahusu kujadiri aina za fasihi kama kazi ya sanaa.

kwa kigezo cha uwasilishwaji wa kazi ya fasihi, tunapata aina mbili za fasihi


  • fasihi simulizi
  • fasihi andishi


fasihi simulizi kwa kifupi hii ni aina ya fasihi au kazi ya fasihi ambayo inawasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo. kwa mfano utambaji hadithi, nyimbo, ngojera na maigizo au drama.

fasihi andishi ni aina ya kazi ya fasihi ambayo mawasilisho yake huwasilishwa kwa njia ya maandishi, kwa mfano riwaya, tamthilia na ushairi


ibrahim mchuchuri.

aina za fasihi aina za fasihi Reviewed by Unknown on May 20, 2017 Rating: 5

1 comment

  1. Fasihi Naipenda Sana Ila Ningependa Kujua Kuna Fasihi Ya Wanyama Au Ya Mimea?

    ReplyDelete