Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii
Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na
kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira.
Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu
jamii, mazingira n.k
Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na
kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii.
Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.
Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha.
Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa
fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.
Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi
za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za
jamii husika.
Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea
hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko
n.k
ibrahim mchuchuri.
Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii
Reviewed by Unknown
on
May 20, 2017
Rating:
No comments