Fasihi ni nini?
Wapo wataalamu mbalimbali
ambao wamekuwa na dhana tofauti tofauti kuhusu maana ya istilahi fasihi na
wamejaribu kutoa maana mbalimbali, hivyo basi katika sehemu hii tutaangalia
baadhi ya maelezo yaliyotolewa na baadhi ya wataalamu wa fasihi kufasili maana
ya fasihi:
Fasihi ni kazi ya sanaa
inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe kwa hadhira au jamii iliyokusudiwa.
Tigiti Sengo na Kiango wanasema, Fasihi ni
mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha wa hadhi na taadhima.
Fasihi yaweza kuelezwa
kwamba, hutegemea msanii ambaye huiumba kwa maneno katika tukio maalum
(Finnegan, 1970)
Ni fasihi inayotegemea
mdomo ktk kutolewa na kuenezwa kwake… (M.L.Matteru, 1979)
Ni aina ya fasihi ambayo
hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa waasikilizaji na
watumiaji waake (Balisidya, 1983)
Fasihi humaanisha fasihi
itolewayo kwa neno la mdomo… (Okpewho, 1992) F.S ni kazi ya sanaa inayotumia
lugha kazi hii ya sanaa huhifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya
masimulizi ya mdomo… (M.Msokile, 1992)
Ni fasihi inayotungwa au
kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia mdomo na vitendo bila
kutumia maandishi (Mulokozi, 1996)
Neno Fasihi linamaanisha
hadithi za jadi, nyimbo, mashairi, vitendawili na methali ambavyo hutolewa kwa
neno la mdomo (Bukenya na Wenzake, 1997)
Sanaa hii iitwayo Fasihi,
inaweza kuhifadhiwa kwa njia kuu mbili: kwa njia ya mdomo na kimaandishi. Aina
ya kwanza, ambayo tunajihusisha nayo katika sehemu ya kwanza inajulikana kama
F.S (Wamitila, 2003) Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap
Fasihi ni kielelezo cha
hisia za mwandishi juu ya mambo yanayomwathiri yeye, kikundi au jamii nzima
anamoishi na kwamba lengo lake kustarehesha au kufunza wasomaji wake. Fasili
hii pia haikidhi maana halisi ya fasihi, je! Kielelezo hicho cha hisia za
mwandishi huwasilishwa kwa kutumia nini?
Fasihi ni maandishi
yanayohusu nchi au bara fulani, maandishi hayo sharti yawe ya kubuni.
Ukiangalia fasili hii ina upungufu kwani fasihi si lazima yawe maandishi
inaweza kuwa ni masimulizi, na si lazima yahusu nchi ama bara fulani, hivyo
fasili hii inapotosha ukweli kuhusu fasihi.
Fasihi ni kazi ya sanaa
inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe au fikra za fanani.
Fasihi ni kitu chochote
kilicho kwenye maandishi. Hii fasili ina mapungufu sana, kwani fasihi si lazima
yawe maandishi, masimulizi pia yanaweza kuwa ni fasihi, lakini piasi chochote
kilichokwenye maandishi ni fasihi kwani fasihi ni lazima kuwa matumizi ya lugha
ya kisanaa.
Fasihi ni sanaa
inayoakisi maisha ya jamii.
Fasihi ni chombo cha
utetezi wa maslahi ya tabaka moja au jingine na kwamba mwandishi ni mtumishi
wake anayejua au asiyejua, atake asitake mwandishi huyo huwa na lengo au
dahamira fulani anayotaka kuionesha,wasomaji wanaweza kuikubali au kuikataa nap
engine kutokana na fani, itikadi ya siasa inayotawala au jinsi mwandishi
anavyoainisha.
Kwa ujumla tunaweza sema
fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa.
ibrahim mchuchuri
Fasihi ni nini?
Reviewed by Unknown
on
May 20, 2017
Rating:
Vizuri sana
ReplyDeleteFasihi kama fasihi ni nini? Kwa wataalamu mbali mbali
ReplyDeleteNingapata mfano wa hiyo fasihi kwa rugha, maana kunarugha ya tafsida na kunaisiyojificha
ReplyDelete